26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Bondia afariki kutokana na kipigo

Buenos Aires, ARGENTINA

Bondia wa Argentina, Hugo Santillan (23),  amefariki kutokana na majeraha aliyopata katika pambano la kuwania mkanda WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu.

Santillano alizimia ukumbuni wakati wa pambano lao lililofanyika Jumamosi lililofanyika Julai 20, nchini Argentina na kumalizika kwa sare.

Bondia huyo alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji wa dharura lakini ilishindikana na akafariki Alhamisi Julai 24.

Katika ukurasa wa Twitter Baraza la Mchezo wa Ngumi Duniani (WBC), liliandika: “ Pumzika kwa amani Hugo Santillano, alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika pambano la Jumamosi lililoisha kwa sare, kwa majonzi tunaungana na familia yake na rafiki zake.”

Santillano amefariki ikiwa ni siku chache baada ya kifo cha bondia wa Urusi Maxim Dadashev.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles