27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Bobby Brown amkumbuka bintiye Bobbi Kristina

Los Angeles, Marekani

Mwimbaji na Mtunzi wa nyimbo  kutoka nchini Marekani Bobby Brown amemkumbuka binti yake Kristina Brown ikiwa ni miaka mitatu tangu afariki dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Brown ameandika ujumbe leo Ijumaa Julai 26 akielezea namna anavyomkumbuka binti yake Kristinna baada ya miaka mitatu ya kifo chake.

“Kila siku nakuweka karibu na moyo wangu, nikifikiria kuhusu vitu vingi ulivyokuwa unafanya, kutoka kuwa msichana mdogo hadi binti mzuri, natabasamu tu, vinanikumbusha ni kiasi gani namkumbuka mtoto wangu mdogo zaidi na zaidi kila siku, unapendwa na unakumbukwa sana.

“Katika kukuenzi, familia yetu imeanzisha Shirika la Hisani la Bobbi Kristina ambalo linafanya vitu kusaidia watu wenye uhitaji, kitu ambacho ungekifanya kama ungekuwa hai.

“Kristina katika siku hii muhimu tunakuenzi, tunakupenda na tunawasha mwanga kukuenzi,” ameandika Brown.

Kristina alifariki Julai 26 mwaka 2016 kwa ugonjwa ‘Pnemounia’ baada ya kuwa mahututi akipumulia mashine kwa miezi sita, ikiwa ni miaka minne baada ya mama yake mzazi Muimbaji marehemu Whitney Houston aliyefariki Februari 11, 2012 kwa ugonjwa wa moyo.

Bobby Brown akiwa na marehemu Whitney Houston na binti yao Kristina alipokuwa mdogo.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles