Elizabeth Hombo, Dodoma       |     Â
Serikali imesema itafanya ukarabati mkubwa katika bonde la Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Josephat Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo ambaye alihoji ni lini miundombinu ya stendi ya mwendokasi itakarabatiwa.
Alijibu swali hilo, Kandege amesema Julai 20 mwaka huu, kandarasi itafunguliwa ili miundombinu ya stendi ya mwendokasi yakarabatiwe.
“Suala lililopo si kuhamisha stendi bali suala ni miundombinu ipi inakwepo pale. Na mpango mahususi ambao serikali inao ni kurekebisha miundombinu ya bonde la Msimbazi na Julai 20 kandarasi itafunguliwa ili miundombinu pale Jangwani iwe na uhakika,”amesema.