23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NYARAKA ZA MAASKOFU KAA LA MOTO KILA KONA

Na ELIZABETH HOMBO – DODOMA


NI kaa la moto. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali kuyaandikia barua makanisa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Romani Katoliki, kuyataka kuomba radhi na kufuta nyaraka zao walizotoa wakati wa Pasaka.

Mjadala kuhusu nyaraka hizo, jana uliibuka bungeni baada ya Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), kutaka maelezo ya Serikali kuhusu hatua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuyataka makanisa hayo kufuta nyaraka hizo na kuomba radhi.

Hata hivyo, swali hilo la Mbatia liligonga mwamba baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kulifuta na kumtaka Waziri Mkuu kutolijibu.

Baada ya kipindi cha maswali, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilitangaza siku kumi kuanzia jana kuishinikiza Serikali bungeni kufuta barua zake kwenda KKKT na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Wamesema kuanzia sasa watahakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ndani ya Bunge, kuitaka Serikali kutoa majibu ya kina kuhusu barua hizo.

Pia kambi hiyo imeitaka KKKT na TEC kutojibu barua hizo hadi Serikali itakapowaomba radhi.

Katika hilo, Naibu Spika, alisema hata Spika Job Ndugai aliwahi kuzuia kiongozi huyo wa Serikali kujibu masuala yanayohusu imani.

“Mtakumbuka Mheshimiwa Kubenea (Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea) aliwahi kumwuliza hapa Waziri Mkuu kuhusu mambo ya dini na Mheshimiwa Spika alizuia suala la kiimani lisijibiwe,” alisema Naibu Spika.

Katika swali hilo, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) alihoji: “Kuna barua wamepewa KKKT na TEC wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresma. Je, Serikali ina lengo gani na inatoa kauli gani kuhusiana na hili?”

MSIMAMO WA WAPINZANI

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wabunge wa upinzani, Mbatia alisema Waziri Mkuu ndiye msimamizi na mdhibiti wa shughuli za Serikali bungeni na swali alilouliza lilitaka kupata majibu kuhusu hatima ya KKKT na TEC.

Alisema swali kwa Waziri Mkuu lilitaka kupata majibu kwa kuwa makanisa hayo yameandikiwa barua ya kupewa siku kumi kufuta waraka wa Pasaka wa KKKT na wa TEC uliotolewa kipindi cha Kwaresma.

“Sisi tunawaomba KKKT na TEC wasiwajibu Serikali halafu waone Serikali itachukua hatua gani kwani nchi hii si mali ya Serikali.

“Waumini wako katika hamaki, viongozi hawa wa dini ni Watanzania na wana haki ya kutoa maoni, Serikali inapaswa kuwaomba radhi waumini.

“Kwa sababu hawa ni wadau wakubwa wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na amani ya taifa letu. Ukiwatikisa hawa leo hii hofu ya usalama ni kubwa sana.

“Waumini wako katika hamaki, viongozi hawa wa dini ni Watanzania na wana haki ya kutoa maoni, Serikali inapaswa kuwaomba radhi waumini. Mamlaka zilizotoa nyaraka hizi ni mamlaka za Bibilia na kama Serikali hii inataka kukanyaga basi,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Abdallah Mtolea, alisema wameamua kuyasema hayo kwa kuwa ni wazi kwamba yatakwenda kuivuruga nchi, kwa sababu taasisi hizo zinaongozwa na viongozi wa kiroho wanaoaminika kuliko wao wanasiasa.

Inaendelea…………… Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles