29.3 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

SAMIA: TUNA KAZI KUBWA KUELIMISHA JAMII KUHUSU FISTULA

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi kubwa kuhakikisha jamii inafikishiwa ujumbe kuhusu tatizo la fistula na athari zake kwa afya ya mama na uchumi kwa ujumla.

Mama Samia amesema hayo leo Alhamisi Juni 7, alipozungumza katika Viwanja vya Hospitali ya CCBRT ambako alifanya ziara kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

“Mliponifata kuomba kurekodi ule ujumbe ambao unasambaa mitandaoni kwa njia ya sauti na video hata sikuwa naelewa kwa kina kuhusu tatizo hili, mkanieleza na sikujua kwamba kwa kuzungumza kule kungesaidia kufikisha ujumbe, kumbe imesaidia, lakini bado ujumbe unahitajika kupelekwa kwa jamii.

“Siku moja nikiwa kwenye mkutano kule Zanzibar wanawake walinifuata na kunihoji kuhusu tatizo la fistula, nikaanza kuwaeleza, utaona namna ambavyo elimu hii inahitajika zaidi hasa katika ngazi ya chini ya jamii tena ile masikini,” amesema.

Awali akizungumza Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans ameiomba serikali kuipunguzia kodi hospitali hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

Naye, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali inakusudia kuirejeshea tena Hospitali ya CCBRT ruzuku kama ilivyokuwa ikipatiwa hapo awali ili kuiwezesha izidi kutoa huduma bora kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,631FollowersFollow
542,000SubscribersSubscribe

Latest Articles