27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Boko Haram wachoma moto kijiji kizima

BORNO, NIGERIA


WAPIGANAJI wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, wamevishambulia vijiji vitatu vya Bulaburin, Kofa na Dalori nje kidogo ya mji wa Maiduguri katika Jimbo la Borno na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, watu 12 wamefariki dunia katika tukio hilo baada ya Boko Haram kuvishambulia vijiji vitatu vilivyoko Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria.

Mashuhuda wanasema wanamgambo wa Boko Haram wanadaiwa kuwasili wakiwa ndani ya magari saba na kuvishambulia vijiji vya Bulaburin, Kofa na Dalori nje kidogo ya mji wa Maiduguri katika Jimbo la Borno.

“Magaidi walifanya mashambulizi makubwa na kuchoma moto vijiji vya Bulaburin na Kofa baadaye wakaendelea hadi kijiji cha Dalori ambako nusu yake kimeshambuliwa na kuchomwa moto,” alisema shuhuda Babakura Kolo, alipozungumza na shirika la habari la AFP.

“Wameua watu tisa Kijiji cha Bulaburin, wawili katika Kijiji cha Dalori, lakini waliposhambulia Kijiji cha Kofa walipora vyakula na kuchoma moto

Takribani nyumba 10,000 zimechomwa moto katika Kijiji cha Dalori.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles