25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Sukari yawabana wafanyabiashara

sugarAsifiwe George na Rehema Abdallah (A3), Dar es Salaam

BODI ya Sukari Tanzania imewataka wafanyabiashara wote nchini kuheshimu agizo la Serikali na kusambaza bidhaa hiyo kwa wananchi pasipo kuihodhi.

Kauli hiyo imetolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwanza, alipoulizwa  na gazeti hili kuhusu baadhi ya wasambazaji wa sukari kuonekana hawatekelezi agizo la Serikali kwa kufuata bei elekezi ya Sh 1,800 kwa kilo.

MTANZANIA lilitembelea maduka mbalimbali Dar es Salaam na kubaini kuwa bado wafanyabiashara wanaendelea kuuza sukari kwa bei ya Sh 2,000 hadi 2,400 kwa kilo moja.

Semwanza alisema kila mfanyabiashara anapaswa kufuata bei elekezi iliyotolewa na Serikali ya Sh 1,800 kwa kilo moja na atakayebainika kukaidi amri hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Bodi ya Sukari Tanzania ilipokutana na waandishi wa habari Machi mwaka huu, ilitoa ufafanuzi kuwa sukari ipo ya kutosha kwa matumizi ya ndani na tumewataka wasambazaji wote watumie bei hiyo elekezi iliyotolewa na Serikali.

“Bodi kwa kushirikiana na sekretarieti za mikoa, inaendelea kufuatilia utekelezaji wa agizo la Serikali la bei elekezi ya Sh 1,800 kwa kilo moja,” alisema Semwanza.

Alisema mahitaji ya sukari kwa mwaka ni karibu tani 420,000 na hadi sasa viwanda vya ndani vimezalisha tani 293,724.94 kati ya 295,070.00 zilizotarajiwa kuzalishwa katika msimu wa mwaka 2015/16.

Semwanza alisema mamlaka za dola hazitasita kumchukulia hatua stahiki za kisheria mfanyabiashara yeyote atakayebainika kukiuka agizo hilo la Serikali kwa kutokuuza sukari kwa bei elekezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles