26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Pamba yawapiga tafu wakulima wa pamba Simiyu

Na Derick Milton, Itilima

Zaidi ya wakulima 1,500 kutoka Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wamepatiwa pembejeo mbalimbali za kilimo kwa ajili ya zao la Pamba vikwemo vinyunyuzi dawa, pamoja na dawa sumu lengo likiwa kupamba na wadudu wanaoshambulia zao hilo wakiwemo funza.

Pembejeo hizo zimetolewa na Bodi ya pamba, ambapo wakulima wengi waliopatiwa ni wale wenye mashamba makubwa kuanzia hekari tano na zaidi, huku bodi hiyo ikibainisha kuwa wamejipanga kuhakikisha wakulima wote wanapata viuatilifu vya kutosha.

Katika zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Said Itaso amesema kuwa, bodi ya pamba imelenga kuhakikisha katika msimu wa mwaka huu wakulima wanajikwamua kiuchumi kupitia zao hilo.

Amesema kuwa malengo bodi katika msimu wa mwaka huu ni kuzalisha pamba tani Milioni moja nchi nzima, huku mkoa wa Simiyu pekee malengo yakiwa ni kuzalisha tani 500,000 (laki tano).

“Kama nchi tunalengo la kuzalisha tani milioni moja huku mkoa wa Simiyu pekee ukiwa na lengo la kuzalisha Tani 500,000 za pamba mbegu hivyo Ili kufikia malengo hayo tumeona tuwaite wakulima wakubwa wa hapa Itilima tuwapatie silaha hizi na wakazalishe pamba ya kutosha,” amesema Itaso.

Ameongeza kuwa wakulima waliopatiwa pembejeo hizo wanatoka katika vijiji vyote 102 vya Wilaya ya Itilima na zoezi hili pia lina lengo la kuwatambua wakulima wote na kutengeneza Kanzidata (Database) za wakulima wote wilayani humo.

Kwa upande Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wilayani humo, Mateso Kiswanu amesema kuwa wilayahiyo imeweka malengo ya kuzalisha tani 23,000 za pamba mbegu ambapo ameishukuru bodi ya pamba kwa hatua walizochukua kuwaletea wakulima pembejeo.

“Kama wilaya tumewekewa lengo na mkoa kuzalisha tani 23,000 za pamba mbegu, na kwa kitendo hiki tunaishukuru Bodi ya pamba kwa kuwapatia wakulima wetu hizi pembejeo kwani mavuno yatakayo patikana yataongeza mapato ya mkulima, halmashauri na taifa kwa ujumla,” amesema Kiswanu.

Mmoja wa wakulima walionufaika na pembejeo hizo kutoka katika kijiji cha Bumera ,Joseph Burai ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa mikakati ya dhati ya kumkomboa mkulima na alisisitiza zoezi hili liwe endelevu.

Aidha, Burai ameshukuru kitendo cha bodi ya pamba kuwaletea viuatilifu pamoja na pampu za kunyunyuzia, ambapo ameeleza kipindi cha nyuma walikuwa wakiangaika kutafuta pampu hizo.

“Tunawashukuru sana bodi ya pamba kwa kutuletea vifaa hivi pamoja na dawa mapema, uko nyuma haikuwa hivyo lakini pia kutuletea dawa na pampu tumeshukuru sana, kipindi cha nyuma tulikuwa tunaletewa dawa tu bila pampu, lakini leo tunashukuru sana tumeletewa vyote,” amesema Burai.

Nae, Isaya Mbembela ameishukuru serikali na bodi ya pamba kwa uwezeshaji wakulima na kusisitiza pia jitihada zifanyike katika kuboresha soko la pamba ili mkulima apate anacho stahiki ili aongeze bidii za uwekezaji katika zao hilo.

Serikali kupitia bodi ya pamba imekuwa na mikakati ya kuhakikisha zao la pamba linaimarika na kuongeza tija katika uchumi wa mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mikakati hiyo ilianza kwa elimu iliyotolewa na balozi wa pamba, Aggrey Mwanri, ugawaji wa Mbegu na kisasa, pembejeo na lengo nikufikia uzalishaji wa tani Milioni moja nchi nzima na tani 500,000 kwa mkoa wa Simiyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles