25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Filamu kuhimiza Watanzania kuangalia filamu

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

BODI ya Filamu Tanzania imesema imeunda Kamati Maalum ya kurudisha Utamaduni wa Watanzania kuangalia filamu katika kumbi za sinema.

Pia, imeanza uhakiki wa vibanda umiza vilivyopo mtaani lengo ni kuonesha filamu mbalimbali katika vibanda hivyo.

Akizungumza Oktoba 4, 2022 jijini Dodoma, wakati akitaja mafanikio iliyoyapata bodi hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Dk. Kiagho Kilonzo amesema Tanzania kuna kumbi chache za sinema na Watanzania hawana utaratibu wakwenda kuangalia filamu.

Amesema kutokana na hali hiyo bodi imeunda kamati maalum ya kurudisha utamaduni wa Watanzania kuangalia filamu katika kumbi za sinema.

“Kuna vibanda umiza ambavyo ni vingi sana, sasahivi kwa sababu kuna filamu nyingi zinaoneshwa kule tupo katika hatua ya kuviwekea utaratibu tumeishaanza kuvitambua.

“Na tayari timu yangu ipo kazini inapita kwa kushirikiana na maafisa utamaduni kujua kila mtaa kuna vibanda umiza vingapi na kuvisajili na baada ya hapo tutavipa utaratibu jinsi gani vinajiendesha,” amesema Dk. Kilonzo.

Pia, amesema bodi inataribu kamati maalum ya kutetea haki za wasanii ambapo malalamiko 22 yamesuluhishwa huku 8 yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema katika sekta ya filamu kumekuwa na mafanikio makubwa kwani nchi imeweza kutangazwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles