23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bobby Charlton apewa heshima Old Trafford

Soccer - FA Youth Cup - Final - Second Leg - Manchester United v Sheffield United - Old TraffordMANCHESTER, ENGLAND

NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Bobby Charlton, amepewa heshima ya jina lake kutumika katika jukwaa la kusini mwa uwanja wa Old Trafford.

Uwanja huo, ambao ulijengwa mwaka 1910, katika jukwaa hilo la upande wa kusini, kwa sasa litajulikana kwa jina la Bobby Charlton, kutokana na mchango wake ndani ya klabu hiyo.

Charlton, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa klabu hiyo, alikuwa mchezaji mahiri wa Man United na hadi sasa ndiye anashikilia rekodi ya ufungaji bora katika historia, hasa katika kupachika mabao, huku akiwa na mabao 249.

Jina hilo jipya litaanza kutumika rasmi Aprili 2, mwaka huu, mbele ya watazamaji 75,000 wakati wa mchezo wa Man United dhidi ya Everton, huku watu maarufu wakialikwa kwa ajili ya utambulisho wa jina hilo.

Charlton alijiunga na Man United kama mchezaji mwanafunzi mwaka 1953 na kuanza kucheza mchezo wake wa kwanza Oktoba 1956, ambapo alicheza jumla ya michezo 758 hadi anastaafu soka.

Mbali ya kuishikilia rekodi ya klabu hiyo ya kufunga mabao mengi, huku mshambuliaji wa sasa ambaye ni nahodha wa klabu hiyo, Wayne Rooney akibakisha mabao 6 kuikamata, Charlton pia alishikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa timu ya Taifa ya England hadi Septemba 2015, alipokuwa na mabao 49 kwa michezo 106 na Wayne Rooney kuivunja kwa kufunga mabao 50.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles