Sauti yamkwamisha Rihanna kufanya shoo

0
695

RihannaNEW YORK, MAREKANI
MPENZI wa zamani wa Chris Brown, Robyn Rihanna, ameweka wazi sababu ya kushindwa kufanya shoo katika tuzo za Grammy, ni kutokana na sauti yake kuwa na tatizo.
Msanii huyo alitoa taarifa ya kuahirisha kufanya shoo hiyo ikiwa ni saa 48 kabla ya kuanza, huku akidai kwamba sauti yake ilikuwa na matatizo hivyo angepoteza ladha ya shoo hiyo.
“Nilikuwa na matatizo ya kiafya siku tatu kabla ya tuzo za Grammy na nilipokwenda kwa daktari wangu aliniambia kwamba natakiwa kupumzika.
“Hata hivyo, nilijiona kwamba ninaweza kufanya shoo, ila ikiwa imebakia saa moja na nusu daktari wangu aligundua kwamba nina tatizo la sauti hivyo ningeweza kusababisha matatizo mengine,” alisema Rihanna.
Msanii huyo amesema amejipanga kuwapa furaha mashabiki wake katika matamasha mengine kama atapata nafasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here