25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Black Mambaz yazikutanisha timu 13 za mpira wa magongo Dar

Na Mwandishi Wetu

TIMU 13 za mchezo wa mpira wa magongo zinachuana katika msimu wa pili wa michuano ya Black Mambaz inayoendelea jijini Dar es Salaam ikihusisha timu za wanaume nane na wanawake tano.

Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Mpira wa Magongo nchini (THA), Kaushik Doshi, amesema michuano hiyo ya siku nne, iliyoanza Alhamisi Agost 8, 2024 inachezwa katika uwanja wa mchezo wa mpira wa magongo uliopo Lugalo.

Doshi amebainisha kuwa michuano hiyo imeandaliwa na klabu ya mchezo huo ya Black Mambaz ya jijini huku ikisimamiwa na THA, huku ikitarajia kumalizika kesho Agost 11,2024.

Doshi amesema timu za wanaume zimewekwa katika makundi mawili, ambapo kundi A linaundwa na Black Mambaz, ambao ni wenyeji, JMK Park, Ngome, na Nyuki ya Zanzibar.

Kundi B lina timu za TPDF, KMKM (Zanzibar), mabingwa wa mchezo huo nchini Moshi Khalsa (Kilimanjaro), na Twende Boys.

Doshi ameongeza kuwa michuano inayohusisha timu za wanawake itashuhudia mechi zikichezwa na wachezaji watano kwa kila timu.

Timu zinazoshiriki katika michuano hiyo ni wakongwe TPDF, Buza Girls, Twende Ladies, Black Mambaz Ladies, na Majani ya Chai.

Katika moja ya mechi za siku ya ufunguzi, wenyeji Black Mambaz walipata ushindi a 4-0 dhidi ya Nyuki katika mechi ya Kundi A.

Mechi yingine ya kundi hilo iliyochezwa Ijumaa ilishuhudia JMK Park wakipoteza 2-1 kwa Ngome, moja ya timu zenye uzoefu kutokana na kushiriki michuano mbalimbali wa muda mrefu.

Katika mechi ya Kundi A iliyochezwa siku hiyo hiyo, Ngome walitoka sare ya 2-2 na wenyeji wa michuano, Black Mambaz.

Mechi nyingine ya kundi hilo iliyochezwa Jumamosi leo asubuhi ilimalizika kwa Nyuki kuichachafya JMK Park na kupata ushindi wa 3-0.

Timu ya JMK Park haikuweza kufua dafu katika mechi nyingine iliyofuata ambapo ilifungwa 3-1 na Black Mambaz, wakati Nyuki ilitoka sare ya bila kufungana na Ngome.

Mechi za siku ya ufunguzi ya Kundi B iliyozikutanisha timu za Twende Boys na TPDF ilikamilika kwa timu hiyo kongwe ya TPDF kuichapa Twende Boys 11-0.

Wababe wa mchezo wa mpira wa magongo nchini, Moshi Khalsa, walipata ushindi murua wa 3-0 dhidi ya KMKM katika mechi ya kundi hilo iliyochezwa Ijumaa asubuhi.

Timu ambazo zitashika nafasi mbili za juu zitafuzu kucheza katika hatua inayofuata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles