23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

TSB yaanzisha ‘Special Mkonge BBT’

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) imeanzisha mradi maalumu wa Jenga Kesho iliyo Bora kupitia zao la Mkonge (Special Mkonge BBT) ambao unahusisha makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge, Saddy Kambona, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TSB kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge, Saddy Kambona, ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TSB kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane kwenye Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Amesema mradi huo unahusisha uongezaji thamani zao la mkonge ambapo makundi hayo hupewa mafunzo ya kuzalisha bidhaa za mkono kupitia zao la mkonge.

Amesema mkonge una manufaa mengi lakini kwa uchache unao mnyororo wake wa thamani ambapo katika programu hiyo maalumu ya BBT wanayaweka pamoja makundi maalumu yakiwamo ya wanawake na vijana na kuwapa mafunzo ya jinsi ya kuzalisha bidhaa za mikono kupitia zao la mkonge.

“Lakini kwa vijana tunajua kwenye eneo la ujenzi bidhaa nyingi za ujenzi zinaweza kuzalishwa na vijana kama kuzalisha ‘gypsum board’ kwa kutumia nyuzi za mkonge.

“Kwa hiyo vijana hii ni fursa nzuri ya kujitengenezea ajira kupitia zao la mkonge kwa sababu tutakuwa na vituo atamizi maalumu kwenye mikoa ya Tanga, Morogoro na Dodoma kwa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar kwenye Chuo cha Mafunzo Zanzibar ambapo tutakuwa tunawapelekea nyuzi za mkonge na kuendesha mafunzo kujifunza njia mbalimbali za kuzalisha bidhaa zenye ubora tupate manufaa ya ajira, kipato na kubadilisha hali za maisha yetu,” amesema Kambona.

Mradi huo ambao ulizinduliwa rasmi Julai 27, mwaka huu Visiwani Zanzibar unasimamiwa na TSB kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Uchumi wa Buluu, Wizara ya Maliasili na Mali Kale na Chuo cha Mafunzo Zanzibar tayari umeanza kufanya kazi kwa kutoa mafunzo na kugawa mkonge tani 9.6 zenye thamani ya Sh milioni 40 kwa vikundi 20 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu visiwani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles