28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Blac Chyna: Nimekusamehe Tyga ila kuwa makini

TygaBADI MCHOMOLO NA MTANDAO
LICHA ya mgogoro wa muda mrefu kati ya msanii kutoka kundi la Young Money, Michael Stevenson ‘Tyga’ na mpenzi wake wa zamani, Blac Chyna, wawili hao wamesameheana ili walee mtoto wao.
Tyga baada ya kuachana na mrembo huyo ambaye alizaa naye mtoto mmoja, aliamua kutoka na mdogo wake Kim Kardashian, Kylie Jenner, lakini msanii huyo alikuwa akimkumbuka mama mtoto wake hivyo akamtaka warudiane lakini mwana dada huyo aligoma.
Juzi mwanamitindo huyo alimsamehe mwenzake. “Nimekusamehe Tyga, nakupa nafasi hii lakini uwe makini sana,” alisema Blac Chyna.
Kwa hali hiyo inaonekana wazi kuwa uhusiano wa Tyga na Kylie Jenner umefikia mwisho baada ya msanii huyo kusamehewa na mpenzi wake huyo wa zamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles