NEW YORK, MAREKANI
STAA wa mitindo na vipindi vya runinga nchini Marekani, Blac Chyna, amemtaka mtayarishaji wa vipindi vyake, Ryan Seacrest, kukutana na familia ya Kardashian ili kumaliza tofauti zao.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 30, yupo kwenye mgogoro na familia kuanzia mama yao, Kris Jenner, Khloe Kardashian na Kylie Jenner.
Blac na familia hiyo wapo kwenye mgogoro tangu alipoachana na kaka yao, Rob Kardashian ambaye alifanikiwa kupata naye mtoto mmoja katika maisha yao, lakini kwa sasa anataka kumaliza tofauti zao.
“Blac anaamini kuna baadhi ya mambo yake hayaendi sawa kutokana na kutofautiana na familia hiyo, lakini kwa kupitia prodyuza wake ambaye pia yupo karibu na familia, hiyo anaweza kwenda kumaliza tofauti hizo.