26.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Spika aunga mkono shindano la wanawake wanene Uganda

KAMPALA, UGANDA

SHINDANO la urembo la wanawake wanene au wenye maumbo makubwa nchini hapa limepata uungwaji mkono kutoka kwa Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi katika jamii na dini wamekosoa lengo la shindano hilo.

Washiriki walisema lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha wanawake wenye maumbo makubwa Uganda na Afrika kwa ujumla kuondokana na unyanyapaa na kujiamini kuwa hata wao ni warembo.

Mabishano kuhusu mashindano ya wanawake wanene walio na maumbo ya kipekee nchini hapa yamechukua mkondo mwingine baada ya Spika Kadaga kubadili msimamo wake wa awali na kuamua kuyaunga mkono.

Hii ni baada ya waandaaji na washiriki katika mashindano hayo kuwasilisha ufafanuzi wao ofisini kwake.

Tofauti na madai kuwa wanalenga kuyatumia kuwa kivutio cha watalii, walisema wanalenga kuondosha unyanyapaa miongoni mwa wenzao.

Kwa mtazamo wao, wanaamini shindano hilo litaondosha fikra za kimagharibi kuwa urembo unamaanisha mtu kuwa mwembamba.

Spika Kadaga ambaye siku mbili zilizopita alipinga vikali mashindano hayo akisema kuwa hatakubali wanawake wa Uganda kudhalilishwa kama vivutio kwa watalii, alibadili msimamo wake baada ya ufafanuzi huo.

“Washiriki wamesema lengo la mashindano hayo ni kuwawezesha wanawake hawa wa Uganda na Afrika kuondokana na unyanyapaa na kujiamini kwamba hata nao ni warembo,” alisema.

Tangu mashindano hayo yalipozinduliwa mapema mwezi huu, wanasiasa, wanaharakati wa haki za wanawake na viongozi wa dini walijitokeza na kuyashutumu vikali.

Aidha walimtaka Waziri wa Utalii, Godfrey Kiwanda ajiuzulu kwa kuongoza katika kuwavunjia wanawake hadhi na heshima yao.

Hadi sasa zaidi ya washiriki 200 kutoka sehemu mbalimbali za Uganda pamoja na nchi jirani ya Rwanda wamejisajili kushiriki shindano hilo.

 Mshiriki anatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 35.

Kwa mujibu wa ufafanuzi wa waandaaji wa shindano hilo la ‘Miss Curvy Uganda’, Uganda si nchi ya kwanza kufanyika, wakitolea mfano Nigeria na kwingineko.

Kuna makundi ya watu ambao tayari yamewasilisha shauri mahakamani kupinga mashindano hayo ambayo yamepangwa kufanyika Aprili.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles