30.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Nyumba ya Michael Jackson yawekwa sokoni

CALIFORNIA, MAREKANI

NYUMBA ambayo inatajwa kwamba ilikuwa inatumika na Michael Jackson kunyanyasa kijinsia vijana wa kiume wenye umri mdogo, imetangazwa kuuzwa.

Nyumba hiyo ambayo ipo mjini California, inadaiwa kuwa na thamani ya dola milioni 31 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 72 za Kitanzania.

Nyumba hiyo inazidi kushuka thamani, mwaka 2016 ilikuwa na thamani ya dola milioni 100 zaidi ya Sh bilioni 233, mwaka 2017 ikawekwa sokoni kwa dola milioni 70 zaidi ya Sh bilioni 163 na sasa ni hiyo dola milioni 31.

Kushuka kwa bei hiyo kunatokana na madai kwamba nyumba hiyo ilikuwa inatumika kwa matendo machafu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wadogo kwa kipindi hicho.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles