29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Biteko asisitiza zebaki kutotumika migodini

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MATUMIZI ya zebaki katika uchimbaji wa madini  umeelezwa kuwa hatarishi kwa afya ya binadamu  hasa kwa watumiaji ambao ni wachimbaji wadogo wa madini pamoja na mazingira yanayoizunguka eneo husika.

Akizungumza wakati wa kufunga maadhimisho ya Siku tatu ya miaka 50 ya taaluma ya Jiolojia  mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Doto Biteko, alisema wizara imeingia mkataba unaozuia matumizi ya zebaki duniani kwani  ni kemikali ambayo si rafiki kwa afya ya mwanadamu pamoja na Mazingira yanayozunguka.

“Saidieni katika kuhakikisha umoja wenu unasaidia taifa hasa katika kutunza rasilimali zetu. Tuungane na serikali kuhakikisha madini yetu yanachimbwa kihalali huku tukizingatia usalama wa wachimbaji, watu wanaowazunguka na mazingira kwa ujumla ili kuleta tija kwa nchi yetu,” alisema.

Alisema jiolojia ni moja ya taaluma inayogusa karibia nyanja zote za maisha na kuwaomba wanajiolojia kushirikiana na serikali katika kuhakikisha mbadala wa zebaki unasisitizwa kama njia moja wapo ya kupunguza athari ambazo zingepelekea uharibifu wa mazingira.

Waziri Biteko alisema taaluma ya jiolojia ni muhimu sana hasa katika sekta ya madini kwani  sekta  hiyo  ni muhimu kwa ajili ya uchumi wa nchi  hivyo kuna kila sababu ya wanajiolojia kufanya kazi zao kikamilifu na kuunga mkono azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Kati na viwanda ifikapo 2025.

“Nendeni mkawe chachu ya mabadiliko ya sekta hii kwa manufaa ya nchi yetu na sio kwa manufaa binafsi. Mkawe waaminifu katika kazi zenu bila hivyo mtakua mnakwamisha watanzania wenzenu hasa wale wanaojipinda kuhakikisha wanapata mitaji ya kuwawezesha kufanya uchimbaji wa madini kikamilifu,” alisema Biteko.

Aidha alisema NEMC watatangaza kipindi cha mpito juu ya matumizi ya Zebaki na kuwataka wadau kutoa ushirikiano stahiki.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk. Samuel Gwamaka alisema matumizi ya zebaki katika uchimbaji wa madini ni hatari kiafya na serikali haiwezi kuacha watu wake wakapoteza maisha kwasababu yakupata faida.

Alisema  serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli ina lengo la kuwafanya wachimbaji wadogo kukua na kuwa wachimbaji wakubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles