23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Birdman aomba radhi kituo cha redio

Birdman kushotoNEW YORK, MAREKANI

BOSI wa kundi la Cash Money, Bryan Williams ‘Birdman’, amewaomba radhi watangazaji wa kituo cha redio cha Breakfast Club kilichopo New York jijini Marekani.

Msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alivamia kituo hicho na kuanza kuwashambulia kwa maneno watangazaji wa redio hiyo na kuwataka waheshimu jina la msanii huyo na kundi lake.

Kutokana na kitendo hicho cha kuingia studio hizo bila taarifa na kuwashambulia watangazaji hao, kupitia akaunti yake ya Twitter amewaomba radhi.

“Jina langu limekuwa likitumika vibaya katika baadhi ya vipindi vya redio, hivyo nilichukizwa na kitendo hicho, lakini nitumie nafasi hii kuwaomba radhi wahusika wote wa redio hiyo,” aliandika Birdman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles