24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 2.7 kumaliza changamoto ya maji Lindi

Na Hadija Omamay, Lindi

JUMLA ya Sh bilioni 2.7 zilizogharamia utekelezaji wa mradi wa maji katika kata ya Tandangongoro Manispaa ya Lindi mkoani humo zimetajwa kumaliza changamoto ya maji katika mitaa saba ya Kata hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Agosti 28, 2021 na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Lindi, Mhandisi Iddi Pazi, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa maji katika ghafla ya uzinduzi wa mradi huo uliofanywa na Mkimbiza Mwenge kitaifa 2021, Luteni Josephine Mwambashi uliofanyika katika kata hiyo.

Pazi amesema kuwa mradi huo wa Maji Tandangogoto una hudumia wakazi zaidi ya 11,310 wanaoishi katika mitaa sita ya kata hiyo ambayo ni Narunyu, Zahanati, Zawiani, Msikitini Tandangongoro na Muungano iliyopo katika kata hiyo ya Tandangongoro.

Amesema miundombinu ya mradi huo pia imesaidia upanuzi wa mradi mwingine wa maji wa Ng’apa vijijini unaohudumia mitaa 7 ambayo ni Mkupama, Mbuyuni, Mapokezi, Mahakamani, kumbaila, Livengula na Cheleweni iliyopo katika Kata ya Ng’apa.

Ameongeza kuwa mradi huo ulihusisha kazi mbali mbali ikiwemo usimikaji wa pampu mbili za kusukuma maji, zenye uwezo wa lita 30,000 kwa saa kutoka kwenye mitambo ya kutibu maji Ng’apa, ulazaji wa mabomba yenye urefu wa mita 26,385, ujenzi wa Tenki moja la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 200,000, ujenzi wa vituo 10 vyenye koki mbili mbili za kuchotea maji pamoja na ufungaji wa vipuli vya kuzimia moto (fire hydrant) mbili na vipuli (fittings) vingine

Hata hivyo Pazi ameeleza kuwa tangu mradi huo uanze kufa ya kazi wananchi wa kata hiyo wameanza kupata maji safi na salama tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia maji kutoka katika visima vya chini ama mifelejini.

Kwa upande wake, Moshi Mabenzi pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuwaletea huduma ya Maji safi na salama katika kata yao pia aliiomba kuongeza vituo vya kuchotea maji katikati ya mitaa ili wananchi waweze kuifikia huduma hiyo kwa urahisi.

“Ukilinganisha na tulipokuwa tunachota maji zamani ni mbali kuliko tunakochota sasa ila tunaiomba serikali wazidi kusambaza mabomba na katikati ya mitaa kwani kwa sasa vilula vingi vipo barabarani tu,” amesema Mabenzi.

Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo wa maji, Kiongozi wa mbio maalum za mwenge wa Uhuru kitaifa 2021 aliwataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu pamoja na vyanzo vya maji ili mradi huo uweze kutumika kwa muda mrefu.

Katika wilaya ya Lindi mbio za mwenge wa Uhuru zimetembekea, zimezindua pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles