29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge wa Uhuru waridhishwa na ujenzi wa Barabara Mtama

Na Hadija Omary, Lindi

MWENGE wa Uhuru Maalum 2021 umeridhishwa na usimamizi wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya kutoka Mtama hadi Mahakama ya Mwazo Mtama yenye urefu wa mita 800 kwa kiwango cha lami unaotekelezwa katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi na Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA).

Akizungumza Ijumaa Agosti 27, 2021 wakati wa uwekaji jiwe la Msingi wa mradi huo, Kiongozi wa Mbio Maalum za mwenge wa Uhuru 2021, Luteni Josephine Mwambashi amewataka wasimamizi wa mradi huo kuendelea kuwa wazalendo kufanya kazi kwa uaminifu ili kila Mtanzania aweze kunufaika na miradi iliyopo katika maeneo yao

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suruhu Hassan inajitahidi kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma muhimu hivyo ni wajibu kwa wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi kufanya hivyo kwa haki na kuwa na moyo mmoja kwa kuleta maendeleo kwa watanzania wote

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Mtama, Dowson Paschal, amesema mradi huo ni kati ya mitano ya barabara iliyotekelezwa na TARURA Halmashauri ya Mtama kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 ambapo umetumia kiasi cha Sh 296,690,000 kwa awamu ya kwanza huku akieleza kuwa kwa sasa mkandarasi ameshalipwa kiasi cha Sh 271,550,000 na kubaki kiasi cha Sh 25,140,00 zitakazolipwa baada ya taratibu za malipo kukamilika

Paschal pia ameongeza kuwa mradi huo umetengewa Sh 80,150,000 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambazo zitatekeleza mradi huo kwa awamu ya pili ya lami na kujenga mifereji ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya M/S BARACON SERVICES CO. LTD wa Lindi amepata na ameshaanza kazi.

Hata hivyo alimueleza kiongozi huyo wa mbio maalum, za Mwenge kuwa kazi zilizofanyika kwa awamu ya kwanza ni kupanua barabara pamoja na kusawazisha barabara mita 800, kuondoa udogo tabaka la juu m³ 300, kuweka tabaka la kifusi tabaka la G45 m³ 1642, kuweka tabaka la kifusi cha kokoto zilizosagwa (CRS) m³ 6,660, kujenga mifereji ya zege na chuma (BRC) m³105.

Aidha, Paschal alieleza lengo kubwa la kujenga mradi huo kuwa ni kusaidia watumiaji wa Zahanati ya Mtama , Mahakama ya Mwanzo Mtama na katika jitihada za kuboresha miji inayokuwa katika Halmashauri yao ambapo Mtama ndio Makao makuu ya Halmashauri hiyo na ni miongoni mwa miji inayokuwa

Katika Wilaya ya Lindi Mbio za mwenge wa Uhuru zimetembelea, zimezindua pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika miradi saba ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles