29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bifu la Tambwe, Ngoma na kisa cha mafahari wawili

YANGA 123

Na ADAMA MKWEPU, DAR ES SALAAM

ILE hadithi  ya mafahari wawili wasiokaa  zizi moja iliyoamia katika klabu ya soka ya Yanga kama isipoangaliwa kwa umakini na kutafutiwa ufumbuzi athari zake zinaweza kuja kuighalimu timu hiyo katika michuano inayoshiriki.

Ni ukweli husiona na shaka kwamba washambuliaji wawili  timu hiyo Amissi Tabwe na Donald Ngoma kwa sasa hawaivu chungu kimoja  ikiwa ni takribani miezi miwili tangu waingie kwenye bifu zito.

Ngoma na Tambwe ndio safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo msimu uliopita 2015/16 ilifanya vizuri zaidi kwa kuwa na  jumla ya mabao 38 yakiwa ni mabao mengi kuliko wengine katika Ligi hiyo.

Pia wachezaji hao wawili waliweza kuisaidia timu hiyo inyakue Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Zaidi ni kwamba Tambwe ni mfungaji bora si msimu uliopita tu bali misimu miwili mfululizo amefanikiwa kuwa bora na kufanya vizuri katika Ligi hiyo.

Hata hivyo Ngoma amekuwa katika wakati mzuri na kiwango bora tangu atue kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani.

Ngome ameweza  kukonga nafsi za mashabiki wa timu hiyo hasa katika michezo ya mwisho ya msimu uliopita pamoja na michezo ya Kimataifa kutokana na juhudi na kipaji chake uwanjani.

Kwa sasa kila mmoja aneonekna kuwa bora zaidi ya mwenzake katika timu hiyo kiasi ambacho kimesababisha kutokea chuki miongoni mwao na kusababisha vikao vya mara kwa mara ili kujaribu kuwatuliza.

Washambuliaji hao hadi sasa hawapati licha ya uongozi wa klabu hiyo kudai kwamba hakuna kitu kama hicho, lakini ukweli ni kwamba Ngoma anaoenekana kuwa na chuki zaidi dhidi Tambwe.

Chuki hiyo alihidhihilisha wakati wakiwa mazoezini walipoweka kambi hoteli ya Rui nchini Uturuki siku moja kabla ya kucheza na TP Mazembe, mchezo ambao Yanga ilifungwa bao 1-0.

Ngoma kwa ghadhabu alimvamia na kumpiga Tambwe na kusababisha kushonwa nyuzi tatu kichwani kutokana na kile kilichodaiwa ni bifu la muda mrefu.

Mzimbabwe huyo wakati akifanya tukio hilo alieleza kwamba mwenzake alikuwa akipendelewa zaidi na kocha wa timu hiyo.

Hata hivyo kitendo hicho kiliibua maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu si mimi na wewe bali hata baadhi ya viongozi wa klabu hiyo hawajafahamu namna ya kufanya ili kuwatuliza mafahali hao.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Hans van Puijm amedaiwa kuitisha vikao kila kukicha hili kuondoa  chuki miongoni mwao lakini ilionekana kazi bure.

Tayari Tambwe ametamka waziwazi kwamba hatoweza kumsamehe mchezaji mwenzake licha ya Pluijm kutumia muda mwingi kuondoa hali hiyo.

Kwa sasa washambuliaji hao hawazungumzi wala kusalimiana kama ilivyokuwa awali ambapo waliweza hata kuombana pasi wakiwa uwanjani na kushirikiana katika kuisaidia timu hiyo.

Kukomaa kwa bifu hilo hadi uwanjani ni nadra kwa sasa kumuona Tambwe akimwomba pasi Ngoma au kumsemesha wakiwa uwanjani.

Kimsingi  ugomvi huo umeonekana kuigawa timu hiyo na kusababisha kuwepo wafuasi upande wa Tambwe na Ngoma.

Mpasuko  huo uliozalisha makundi mawili ya wazawa na wazimbabwe umepunguza hamasa na hali ya kujituma ndani ya timu hiyo.

Kufanya vibaya kwa timu hiyo katika michezo ya kimataifa kunasababishwa na vitu vingi ikiwemo kitendo cha wachezaji kujigawa ndani ya timu hiyo.

Licha ya ujio wa Obrey Chirwa ili kuongeza nguvu katika safu hiyo, inahitaji zaidi ushirikiano wa Ngoma na Tambwe ili kuimarisha safu hiyo.

Bado Tambwe na Ngoma wanayonafasi ya kuendelea kufanya vizuri kama hawatakuwa na bifu kutokana na umahiri wao wanapokuwa uwanjani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles