22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Bibi anayedaiwa kuua mjukuu aomba huruma ya mahakama

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA Esther Lymo (47) anayedaiwa kumuua mjukuu wake, Naomi John (7), ameomba huruma ya mahakama imwachie huru.

Amedai alimchapa mjukuu wake huyo kwa kumkanya na makovu aliyokutwa nayo mwilini, alitoka nayo kijijini sababu alikuwa anachunga mbuzi.

Ushahidi wa Esther umekanganyana na ushahidi wa mwanaye, Jackline Kesi ambaye alidai Naomi alipotoka kijijini alikuwa na mapunye kichwani, mchafu na kidonda sikioni.

Jackline na Esther walitoa ushahidi wa utetezi jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Msajili Pamela Mazengo.

Akijitetea, Esther alidai kwamba vidonda na makovu katika mwili wa Naomi yàlitokana na shughuli za uchungaji mbuzi kijijini kwao mkoani Kilimanjaro.

Alidai Naomi na Andrew John ni watoto wa dada yake na aliwachukua kuishi nao baada ya kuombwa awasomeshe kwa kuwa dada hakuwa na uwezo.

Mshtakiwa alidai aliweza kukaa na watoto hao kwa miezi 10 nyumbani kwake Toangoma mbako pia kuna mapori kama kijijini kwao Moshi.

“Watoto hawa ni watundu sana, huwa wanakimbizana na kucheza vichakani, hivyo ndiyo maana mwili wake ulikuwa na vidonda na makovu, sijamuua Naomi, nilikuwa nawapenda, naomba mahakama iniachie huru.

“Machi 25, mwaka 2016 wakati natoka kufanya usafi saluni kwangu, nilielezwa na Andrew kuwa Naomi ameamka, amejikojolea yupo barazani.

“Nilimwambia Naomi akapige mswaki, nikaingia ndàni, lakini aliendelea kukaa barazani, Andrew aliniambia hapigi mswaki anachezea maji, nikaongea kwa sauti kwamba nikitoka ndani nitàmchapa, nilipotoka Naomi akakimbia nikamwambia Andrew amkamate.

“Alipoletwa nilichuma fimbo katika mti wa mparachichi na kumchapa kwa nia ya kumkanya kama mzazi, wakati namchapa Naomi akasema amechoka, mi nilidhani ni utani kwa sababu ya kukimbia na ujeuri wake, nilimnyànyua na kumweka barazani, nikaenda kutafuta dawa, nilivyorudi nilikuta amelegea sana, hivyo nikachukua gari ya jirani na kumpeleka hospitali Temeke,” alidai.

Ester alidai daktari aliwaambia Naomi alikuwa amepungukiwa damu sababu walikaa naye bila kumtibu malaria, alikaa kwa daktari akasikia akihema kwa nguvu, hakuelewa kitu hadi daktari alipowaeleza kuwa ameshafariki.

Alidai kuwa wakiwa hospitàli, polisi walikuja kumchukua na kupelekwa Kituo cha Polisi Maturubai na baadaye Charambe na Aprili 4 mwaka 2017 akafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Naye Jackline katika ushahidi wake wa utetezi, alidai Naomi alikuja akiwa na mapunye kichwani, mchafu na kidonda sikioni.

Shahidi huyo alipobanwa kwa maelezo aliyotoa polisi, alidai aliwaeleza polisi kuwa mama yao (mshtakiwa) ni mkali sana na alikuwa akimpiga sana Naomi.

Wakati akijibu maswali ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Cecilia Mkonongo, Jackline alidai kabla ya mama yake kumchapa Naomi, alikuwa ameshalegea sana na baada ya kumchapa alikuwa amelegea kabisa.

Alidai, alipoishiwa nguvu alimuona mama yake akichukua maji ya moto na kummwagia Naomi katika vidonda na ndipo akaishiwa nguvu na kumbeba kumpeleka hospitali.

“Mimi ndio nilimbeba Naomi wakati tunaenda hospitali, tukiwa njiani nilisikia Naomi akivuta pumzi kwa nguvu, sikujua kama alikuwa amekufa hadi tulipomfikisha hospitali,” alidai Jackline.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles