Na Shomari Binda, Musoma
Timu ya Biashara United imeingia miataba wa Sh milioni 200 na jampuni ya Macron Tanzania ya kutengeneza na kusambaza jezi za timu hiyo.
Mkataba uliosainiwa mbele ya Raandrshi wa Habari na viongozi wa timu ya Biashara United na Macron utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Moja ya kipengele kulichopo kwenye mkataba huo ni pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji zikiwemo jezi, mabegi ya safari, kofia, skafu pamoja na jezi za mashabiki.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Katibu Mkuu wa timu ya Biashara United, Haji Mtete, amesema kampuni ya Macron imepata tenda hiyo baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na timu hiyo mwezi Mei.
Amesema kampuni mbili zilizokuwa zikiwania tenda hiyo ni Macron na Vunja Bei lakini Macron ndiyo imefanikiwa kupata nafasi hiyo ambayo amedai imekuja wakati muafaka.
Mtete amesema msimu wa mwaka 2021/2022 mashabiki watarajie kupata jezi za kiwango na kwa muda muafaka kabla ya kuanza msimu na kudai uongozi umejipanga kufanya mengi mazuri msimu mpya.
“Uongozi umejipanga kufanya vizuri kwenye maeneo mengi msimu ujao na umeanza na hili la kupatikana kwa vifaa vya michezo mapema kabla ya kuanza msimu ujao,” amesema Mtete.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Macron Tanzania, Duleiman Isihaka amesema watahakikisha vifaa vinafika kwa wakati muafaka na kuwafikia wahusika.
Amesema wanaushukuru uongozi kwa kuwaamini na kwamba hawatawaangusha kwenye kile walichokubaliana kwenye mkataba huo.