28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

TFS yazipiga tafu shule, ofisi Muheza kwa kuzipa samani za Sh mil 17.4

Na Amina Omary, Tanga

Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) shamba la Lunguza lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga wametoa msaada wa madawati, viti na meza vyenye thamani ya Sh milioni 17. 4.

Msaada huo ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari tatu pamoja na ofisi za watendaji kata mbili zilizopo wilayani Muheza.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo, Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti Longuza, Ellyneema Mwasalanga amesema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma.

“Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari,” amesema Mwasalanga.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo, aliishuku TFS kwa namna walivyothamini elimu ya Watoto wa kitanzania na hivyo kwa msaada huo wataweza kuboresha utoaji wa elimu.

“Niwaombe wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi,” amesema Bulembo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles