Biashara United kujipima na Alliance

0
568

Na Shomari Binda, Msoma

Timu ya Biashara United ya Mara imeelekea jijini ni Mwanza kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu ya Alliance ikiwa ni maandalizi kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Biashara United itashuka dimbani hii leo kucheza mchezo huo kabla ya kucheza michezo mingine ikiwa ni kujiweka sawa kwa ajili ya ligi kuu

Akizungumza kuelekea michezo hiyo ya maandalizi, Kaimu Katibu wa timu hiyo, Japhet Nzige, amesema michezo hiyo itamsaidia kocha, Francis Baraza, kuona utimamu wa wachezaji wake.

Amesema maombi ya kocha ni kutafutiwa michezo ya maandalizi na uongozi unaendelea na mazungumzo na timu nyingine ili kuweza kupata michezo hiyo.

Nzige amesema matarajio ni kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi pale itakaporejea na ili kufanya hivyo ni timu kuwa imara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here