30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bi Kidude kukumbukwa Unguja na Dar

Bi Kidude2NA RUTH MNKENI

FILAMU ya maisha ya Bi Kidude inatarajiwa kuzinduliwa Aprili 16 visiwani Zanzibar katika Ukumbi wa ZanCinema mjini Unguja.

Filamu hiyo pia itazinduliwa  Dar es Salaam Aprili 19 mwaka huu.

Mwandaaji na mtayarishaji wa filamu hiyo, Andu Jones, alisema filamu hiyo itabeba ujumbe kuhusu maisha ya bibi huyo na kueleza kifo chake ikiwa katika lugha ya Kiswahili.

“Bi Kidude alikuwa msanii maarufu hapa nchini na dunia nzima kwa ujumla hivyo kila mtu anataka kujua na kusikia nini kimefanyika katika maisha yake,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusufu Mahmoud, alisema Bi Kidude alikuwa akipokea 10%  ya faida kutokana na mauzo ya kazi zake hivyo watayarishaji hao wapeleke sehemu hiyo ya faida kwenye Chuo cha Mafunzo ya Muziki wa Nchi za Jahazi kilichopo Mji Mkongwe ili kusaidia kuwaendeleza wanamuziki wa kike wanaosoma pale.

“Wakati huu ambao Zanzibar inasonga mbele, ni vyema kuwakumbuka mashujaa waliopita na kupeleka utamaduni wa Mzanzibari kwa watu wengine duniani,” alisema Mahmoud.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles