25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BENKI YA NMB YAWEZESHA WAKUNGA MUHIMBILI

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kupitia ufadhili wa Benki ya NMB, wametoa huduma bure kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kama sehemu ya maandalizi ya Siku ya Wakunga Duniani.

Benki ya NMB ndio wadhamini wa tukio hilo, lililowezesha mamia ya Watanzania kupata huduma kupima afya zao bure na hivyo kuendelea na dhana ya benki hiyo ya kuwajali Watanzania wa kada mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika viwanja vya Hospitali ya Taifa Muhimbili, jirani na jengo la watoto, Mwenyekiti Msaidizi wa Chama cha Wakunga Tanzania Tawi la Muhimbili, Elizabeth Thawe, aliwataka wananchi kujitokeza katika eneo hilo ili kuweza kupata huduma hizo za afya bure.

Huduma walizotoa bure ni pamoja saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti, elimu kuhusu lishe bora, shinikizo la damu (BP), sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji watoto kwa akinamama.

“Kuelekea maadhimisho ya siku yetu, tumejitolea kupima afya bure kwa wananchi wote watakaojitokeza katika eneo hili…huduma zinazotolewa bure leo ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti, tunatoa elimu kuhusu lishe bora, tunapima shinikizo la damu (BP), tunapima sukari mwilini na elimu ya unyonyeshaji,” alisema Thawe.

Alisema huduma hizo zinatolewa na wanachama wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) tawi la Muhimbili kwa kushirikiana na wengine kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na vyuo vyote vya afya vinavyozunguka Hospitali ya Muhimbili.

Alisema mbali na kutoa huduma hizo bure, siku ya pili ya maadhimisho watafanya kongamano la kisayansi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku hiyo muhimu kwa wakunga. Aidha, aliishukuru Benki ya NMB ambayo ni wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo pamoja na makampuni mengine yaliyojitokeza kusaidia kufanikisha shughuli hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles