30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya NMB yatenga bilioni 700/- kusaidia miradi

Na GUSTAPHU HAULE

-PWANI

BENKI ya NMB imetenga fedha kiasi cha Sh bilioni 700 kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali pamoja na kusaidia kutoa mikopo kwa wawekezaji mbalimbali.

Mbali na fedha hizo lakini pia Nmb imeliwezesha Shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kununua vifaa mbalimbali  na vifaa vingine vya umeme kwa gharama ya Sh bilioni 54.

Mkuu wa kitengo cha biashara na miradi ya Serikali Vicky Bishubo, aliyasema hayo  katika maonyesho ya bidhaa za viwandani katika viwanja vya mkuu wa mkoa wa Pwani.

Bishubo, alisema kuwa NMB inashirikiana na Serikali pamoja kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo  pamoja na wawekezaji mbalimbali wanaokujua nchini kwa ajili kuwapa fedha za mikopo ili waweze kukamilisha miradi yao kwa njia rahisi.

“Benki ya NMB imetenga mtaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 700 kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya Serikali ukiwemo mradi wa reli ya kisasa na mingine lakini pia fedha hizo pia zitasaidia wawekezaji ili kurahisisha namna ya kuendeleza miradi yao,” alisema Bishubo

Aidha alisema ukiachia mbali kutengwa kwa fedha hizo lakini pia mpaka sasa NMB imetoa dhamana zenye thamani ya Sh bilioni 44 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa REA hapa nchini na kwamba pamoja kutoa fedha bado wanaendelea kujipanga ili kuweza kufikia Kila jamii.

Kutokana na hali hiyo aliwaomba wawekezaji mbalimbali waliopo nchini pamoja wale ambao wamejitokeza kushiriki maonyesho ya bidhaa za viwanja mkoa wa Pwani watumie Benki ya NMB kwa kuwa ndiyo benki ambayo imejikita zaidi katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa Kati kupitia viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles