27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Benki ya Dunia yatoa bilioni 600 kusaidia elimu, miradi ya maendeleo

Anna Potinus, Dar es Salaam



Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na Sh Bilioni 680.5 za Kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, vyumba vya watumishi na kununua vifaa vya kufundishia.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dk. Hafez Ghanem leo Ijumaa Novemba 16, alipokutana na Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam ambapo amesema benki hiyo inaendelea kufadhili miradi mbalimbali nchini yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.2 sawa na zaidi ya Sh Trilioni 13 za Kitanzania.

Aidha Dk. Ghanem amesema katika mazungumzo baina yake na Rais Magufuli wamejadili juu ya maendeleo ya miradi hiyo na kazi nzuri ambayo inafanywa na Tanzania kuimarisha uchumi.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano na uhusiano mzuri na Tanzania na ameahidi kuendelea kukuza uhusiano huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha zote zinatolewa kwa ajili ya miradi na maendeleo na zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa.

“Namshukuru Dk. Hafez Ghanem na Benki ya Dunia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Tanzania, hizo Dola milioni 300 ambazo baadhi ya watu wasiotutakia mema walisema zimefyekelewa mbali, anasema zitaletwa na na pia Benki ya Dunia imetoa Dola bilioni 5.2 ambazo zinafadhili miradi mbalimbali ya elimu, nishati, barabara, kilimo, afya na maji, ni miradi mikubwa na mingi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles