26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mradi kuboresha elimu ya mafunzo ya ufundi stadi waja

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAMTanzania imeingia katika mradi wa kuboresha elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (BEvAR II) utakaogharimu Dola za Marekani milioni 1,500 ambao utasaidia kupata wahitimu waliobobea katika fani mbalimbali za ufundi.

Akizungumza katika kufungua warsha ya siku tatu ya mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo, amesema serikali itaandaa takwimu za wahitimu zitakazosaidia upatikanaji wa ajira ndani na nje ya nchi.

“Niwashukuru serikali ya Korea kwa kufadhili mradi huu na sisi kama serikali tunaahidi kuutekeleza kama yalivyo mapendekezo yaliyoletwa na warsha hii,” amesema Akwilapo.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka wizara hiyo, Dk. Noel Mbonde, amesema mradi huo utasaidia kuongeza nguvu kazi wakati nchi inaingia uchumi wa kati kupitia viwanda.

Amesema kupitia mradi huo wanatengemea sasa kupata wahitimu ambao wana uwezo wa kushindana kitaifa na kimataifa kutokana na kuzibwa kwa pengo lililokuwapo.

“Mradi huu utakwenda kuwajengea uwezo wakufunzi wa taaluma ya mafunzo ya ufundi stadi na kuziba pengo lililokuwa likisababisha wahitimu wetu kukosa ubora,” amesema Dk Mbonde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles