25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Benki ya Azania yadhamini Kids Run Dar

mtanzania kila siku safi.inddNA ESTHER GEORGE, DAR ES SALAAM

BENKI ya Azania imeingia makubaliano na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kuendesha mashindano ya riadha kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 yajulikanayo kama Kids Run Dar es Salaam yatakayofanyika Juni 5.

Hafla ya makubaliano hayo ilifanyika jana na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Benki hiyo imewekeza shilingi milioni 130 kwa ajili ya mbio hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania, Godfrey Dimoso, alisema benki hiyo inamilikiwa na Watanzania na wamejitosa kudhamini mbio hizo baada ya kukubaliana na RT.

“Hili kwetu ni tukio la kihistoria kwa kuwa benki yetu ni ya kwanza kudhamini riadha tukiwa sekta binafsi, hivyo tumekubaliana na wenzetu wa RT kushirikiana katika hilo,” alisema Dimoso.

Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa RT, William Kalaghe, alisema ni mara ya kwanza mashindano hayo kupata wadhamini nje ya Serikali, hivyo itasaidia katika kukuza vipaji vya watoto.

“Hili ni tukio la kihistoria kwetu RT kupata mdhamini nje ya Serikali, tunatarajia watoto zaidi ya 2,000 watashiriki mbio hizi.

“Miji mingi duniani imekuwa maarufu kutokana na riadha, nasi tunaamini kuwa mbio hizi zikisimamiwa ipasavyo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza mji wetu wa Dar es Salaam,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda, aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema watoto wengi wana vipaji, lakini hawapati fursa ya kuendelezwa.

“Kama hatujawekeza kwa watoto, hatuwezi kuendelea kama taifa, michezo si burudani pekee, bali pia ni uchumi wa mataifa mbalimbali, sisi tunazidi kushuka kwa kuwa hatuoni faida ya michezo, lakini tukijipanga vema tutaondokana na uhalifu, vijana watalitangaza taifa na pia kupunguza tatizo la ajira,” alisema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles