23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mamilioni ya Farid Mussa yanukia Azam

FARID MUSSANA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Azam FC umeeleza kuwa tayari kukaa meza moja na klabu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania, kuhusu usajili wa winga wao Farid Mussa.

Winga huyo amefuzu majaribio ya awali Deportivo Tenerife na sasa Azam inataka kukaa meza moja na uongozi wa klabu hiyo kufanya makubaliano.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Idrissa Nassor, alisema wanamwombea Mungu kijana wao amalize vema majaribio yake kwani tayari amefanikiwa katika hatua mbili za awali.

Alisema baada ya taarifa hizo watakutana na viongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo na kusikiliza ofa yao ya kumnunua winga wao.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili… sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa uamuzi,”  alisema Nassor.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles