24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ben Pol, Kiba, Vanessa Mdee, Fid Q kuwasha moto Coke Studio Africa

Ben-Pol_fullvanessa-620x400alikiba1fid-qNA MWANDISHI WETU

WASANII nguli wa muziki nchini, Ben Pol, Ali Kiba, Fid Q na Vanessa Mdee, wataungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya  burudani ya muziki, maarufu kama Coke Studio Africa litakaloanza mapema wiki ijayo.

Onyesho la mwaka huu ni tofauti na yaliyopita kwa kuwa litaendana na mabadiliko yaliyopo katika muziki duniani ‘Kolabo’.

Kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti.

Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni, sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko ambapo safari hii utawawezesha wasanii husika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji.

Wasanii wengine watakaokuwa kwenye onyesho hilo litakaloanza kuonekana kwenye luninga Oktoba 10, mwaka huu ni Wangechi na Victoria Kimani wa Kenya, Maurice Kirya (Uganda), mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, 2Face.

Kwa mujibu wa waandaaji, onyesho kwanza litarushwa kupitia kituo cha televisheni cha Clouds Oktoba 10 kuanzia saa 12 jioni.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles