22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

BEN POL BADO AZIWAZA NDOTO ZA TREY SONGS

Na JESSCA NANGAWE

MKALI wa R&B, Bernad Paul maarufu kama Ben Pol, amesema ndoto zake za kufanya kazi na mastaa wakubwa wa Marekani kama Trey Song na wengine bado zipo wazi na ni moja ya mikakati yake ya mwakani.

Ben Pol ambaye hivi karibuni alipata dili na kusafiri hadi Ufaransa, baada ya kupata dili la kuwa balozi wa kampuni moja inayojihusisha na mambo ya haki za binadamu, alisema baada ya mwaka huu kuwa ‘busy’ sasa anajipanga vyema mwakani.

Akizungumza na MTANZANIA, Ben Pol, alisema tayari mikakati ya kufanya kazi na mastaa wakubwa Marekani alijiwekea na kilichobaki ni utekelezaji na anajipanga kutimiza malengo hayo.

“Ni mipango yangu ya muda mrefu na lazima niitimize, nimpongeze mtu kama Diamond ambaye ameonekana kutimiza ndoto zake kwa kufanya kazi na mastaa wakubwa kama Rick Rose na Neyo, naweza kusema imenisukuma zaidi kuhakikisha na mimi natimiza hilo, hii ni moja ya mipango yangu ya mwaka unaoanza,” alisema Ben Pol.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles