Belle 9: Siwezi kuwa na uhusiano na ‘mamama’

Belle 9NA THERESIA GASPER

MSANII wa RnB kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Abednego Damian ‘Belle 9’, amefunguka kuwa hana hobi ya kujihusisha na masuala ya kimapenzi na wanawake waliomzidi umri.

Belle 9 aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya baadhi ya wasanii wenye umri mdogo kupenda wasichana wenye maarufu wenye umri mkubwa kwake jambo hilo halina nafasi.

“Nafahamu mapenzi hayachagui yanaweza kumtokea mtu yeyote lakini kwangu haliwezi kutokea kwa sababu sitarajii kuwa katika uhusiano na dada yangu ama mama yangu mtu mzima kwangu namfananisha na dada na mama yangu hivyo siwezi kuwa nao kimapenzi,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here