24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Belle 9, Hemed, Izzo B jukwaa moja

bhemed_phdNA OSCAR ASSENGA, TANGA WASANII wa muziki wa Bongo Fleva, Abelnago Damiani ‘Belle 9’, Hemed Phd na Izzo Business, wanatarajiwa kutoa burudani katika onyesho maalumu la siku ya wapendanao lililopewa jina la Red &White Party mkoani Tanga. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa onyesho hilo, Mbwana Imamu, alisema maandalizi yote yamekamilika na wasanii wataripoti mkoani humo Februari 13 mwaka huu. Mbwana alisema lengo kubwa la onyesho hilo ni kuwapa burudani
wakazi wa Tanga katika siku hiyo muhimu na maalumu. “Wadau wa muziki wa kizazi kipya tunaomba wajitokeze kwa wingi Februari 15 katika ukumbi wa Club Lacasa Chika,” alisema Imamu. Imamu alisema kutakuwa na burudani zaidi kutoka kwa wasanii chipukizi wa mkoa huo ambao ni Man Sasha, Kidani, Meratha, Voicer na Fat Zinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles