23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bella: Uongozi ni tatizo kwa wasanii

Na GLORY MLAY

MSANII wa muziki Bongo Fleva mwenye asili ya Congo, Christian Bella, amesema kikwazo cha wasanii wengi kushindwa kufikia malengo yao ni kutokana na kukosa uongozi wa kusimamia kazi zao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bella alisema kuwa kila msanii ana lengo la kwenda mbali zaidi hasa kazi zake zisikike kimataifa lakini tatizo lipo kwenye uongozi.

“Muziki wetu bado una matatizo mengi ndo maana unaona kuna wakati unahitaji kufanya kitu lakini unashindwa, hakuna msanii asiyependa kufika alipofika Diamond, Aly Kiba na wengine, kila mtu anataka lakini tatizo ni kukosa uongozi.

“Kila msanii huwezi kutumia pesa yake ya mfukoni kutengeneza video, hautaweza kufika popote, uongozi ndio kila kitu bila hivyo hatuwezi kufika kokote,” alisema Bella

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles