25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

BEKI SIMBA AWACHONGEA NGOMA, TAMBWE

Na ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM


BEKI wa zamani wa Simba, Fikiri Magoso, ni kama ameisajilia Yanga baada ya kusema ili timu hiyo iweze kutetea taji lake, haina budi kuwapiga chini wachezaji wanaokula mishahara ya bure na kusajili vifaa.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, Magoso alisema Yanga ya sasa ina wachezaji wengi wasiotumika ipasavyo kutokana na kutokuwa kwenye kiwango bora, hivyo ni wajibu wa klabu hiyo kuwatema na kusaka majembe yenye faida.

Alisema uwepo wa idadi kubwa ya wachezaji wasio na faida, kunaiongeza klabu hiyo matumizi yasiyo na lazima, kwa kuwa wanahitaji kulipwa mshahara, malazi lakini pia inapotokea wamepata matatizo wanahitaji kuhudumiwa kitu ambacho ni hasara.

“Hiki ni kipindi cha Yanga kuondoa wale wote ambao ni wafanyakazi hewa na kuwaleta wachezaji wanaojua majukumu yao, iwapo kama wanahitaji kweli kutetea taji la ubingwa msimu huu, tofauti na hapo watausikia tu watu walionao wengi wao si watendaji kazi.

“Ukikiangalia kikosi cha Yanga kuna wachezaji kama Juma Mahadhi, Hajji Mwinyi, Antony Matheo, Buruhani Akilimali, hao ni wazawa, ukija kwa wageni yupo Amissi Tambwe na Donald Ngoma, ambao wanaonekana ni wagonjwa na haijulikani lini watarejea uwanjani,” alisema.

Alisema ufike wakati kwa klabu za Tanzania kuacha tabia ya kusajili wachezaji kwa ajili ya kuzikomoa nyingine pasipo kujua afya zao au historia za maisha yaliyopita, akisema tabia hiyo imekuwa ikiziingiza katika hasara kubwa.

“Hii tabia ya kusajili ili mradi, ndiyo sababu inasababisha Yanga kuwa na wachezaji wengi ambao wanaishia kukaa tu, nawashauri hili dirisha dogo walifanyie kazi, wapunguze wale watendaji kazi hewa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles