29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

KOCHA YANGA AITUMIA UJUMBE MZITO SIMBA

Na ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BAADA ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City, Yanga imemwashia taa nyekundu hasimu wao Simba, ambapo benchi la ufundi la timu hiyo limesema sasa limezindua rasmi harakati za kusaka taji la msimu huu.

Yanga iliibuka na ushindi huo mzito dhidi ya Mbeya City katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara lililopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yaliifanya Yanga iendelee kusalia katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20, nyuma ya Azam FC iliyoko nafasi ya pili na pointi 22 sawa na vinara Simba walioko kileleni kutokana na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema wana matumaini ya kuishusha Simba kileleni kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

“Ikitokea Simba wakapoteza mechi tu wajue hawana tena nafasi ya kuchukua taji na kama ikitokea tukawa na pointi sawa basi wajue ubingwa si wao kwani timu yetu ina uhakika wa kufunga mabao mengi.

“Kwa sasa wao wametuzidi mabao sita ambayo kwa kasi tuliyokuwa nayo hivi sasa ya ufungaji wajue kabisa tuna nafasi kubwa ya kuwakuta na kuwapita na hiyo ni ishara kwamba taji la Ligi Kuu msimu huu tutaendelea kulimiliki, idadi hii ya mabao ni salamu kwao,” alisema.

Kama Simba itafanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, hiyo itakuwa ni baada ya kupita miaka mitano ambapo mara mwisho ilikuwa msimu wa 2011-12.

Kwa upande wa Yanga, endapo itafanikiwa kubeba taji hilo msimu huu, hiyo itakuwa kwa mara ya nne mfululizo, kwani tayari imefanya hivyo mara tatu baada ya kunyakua msimu uliopita.

Katika michezo yake 10 ya Ligi Kuu msimu huu, Yanga imefanikiwa kushinda tano, sare tano, huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.

Simba yenyewe kupitia mechi 10 ilizocheza hadi sasa, imeshinda sita, sare nne, lakini haijapoteza mchezo wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles