23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

BATA LA DIAMOND LILIVYOFUNGA MWAKA 2017

Na CHRISTOPHER MSEKENA

TUKIWA tumebakiza siku moja kuupokea mwaka mpya, leo tunaendelea kukupa matukio yaliyotingisha mwaka 2017. Kati ya mengi yaliyotokea, wiki hii kubwa ni familia ya mwanamuziki Diamond Platnumz kula bata ndefu kusherehekea siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya mtoto wake wa pili, Nillan.

Sherehe hiyo ilifanyika siku ya Jumapili, nyumbani kwake, Pretoria, Afrika Kusini huku ikitengeneza matukio yaliyozua gumzo kwenye tasnia ya burudani kwa wiki nzima. Hapa nakusogezea matukio hayo.

BABA YAKE MDOGO

Baada ya kufunga ndoa, mama Diamond na mumewe walielekea Afrika Kusini kwa mapumziko ambapo huko ndiko ilikofanyika sherehe ya Nillan.

Kiu ya wengi ilikuwa ni kuona kama Diamond atatoa ushirikiano kwa baba yake huyo anayeitwa Shamte ukizingatia ni kijana kama yeye.

Kuonyesha kuwa Diamond hana tatizo na baba yake huyo mpya, wote walishirikiana kufungua zawadi hivyo kuweka picha nzuri kwa jamii tofauti na ilivyodhaniwa.

MAKULUSA YATIKISA

Ngoma mpya ya Rayvanny aliyofanya na Dj Maphorisa (Makulusa) ilikuwa wimbo mkuu katika bata hilo, mbali ya memba wa WCB kama vile Rich Mavoko, Harmonize, Queen Darleen, Romy Jons, Zari, Diamond na mama yake walikuwa wanashinda kuucheza.

Video zinazoonyesha wakiucheza wimbo huo ni moja ya vitu vilivyokuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

BABA AMALIZA BIFU

Itakumbukwa kuwa H Baba amekuwa akionyesha wazi kumchukia Diamond Platnumz hali iliyofanya awe kwenye vita na mashabiki wake, lakini wiki hii staa huyo wa singo ya Poteza ameamua kuweka pembeni tofauti zao na kuisifia kapo ya Diamond na kuahidi kutoa ng’ombe watano walionona.

Chini ya picha ya Diamond na Zari waliyopendeza kwa mavazi meusi, H Baba aliandika: “Mmetokelezeiyaa kinyama mmependezana, mnaendana Allah awasimamie ndoa ifungwe awe wako kwenye hesabu ya Mwenyezi Mungu.

“Nitatoa ng’ombe watano wakubwa kabisa wa Kisukuma waletwe Dar, huo ndiyo uwezo wangu na hicho ndicho nitajaaliwa na Mwenyezi Mungu, nakutakia maandalizi mema ya ndoa yako.

Hongereni kwa kupendana msiyempenda atatoa ng’ombe watano, naheshimu mahusiano ya Mtanzania mwenzangu, mimi ni mzalendo nimekataa kuwa kaa.”

ZARI AMJIBU MOBETTO

Wiki iliyopita  wazazi wenza wa Diamond (Zari na Mobetto) walitupiana vijembe wakiwa nchini Uganda lakini Boss Lady alikaa kimya kwa muda mpaka juzi alipoamua kumjibu Hamisa kupitia mtandao wa Snapchat.

Zari alimjibu Mobetto kwa kusema: “Unaweza ukawa unaposti picha zote za zamani lakini nimeshakuwa na amani na makosa yake yaliyopita, siwezi kubadilisha kile kilichotokea, naendelea kutengeneza mustakhabali wa maisha yangu ya baadaye.

“Mmekuwa mkiongea kuhusu laana, ulijua vyema kwamba Diamond alikuwa mwanamume wa mtu mwingine na familia lakini uliamua kupanua miguu yako na kupata mimba, unadhani laana itanifuata mimi, nimefanya nini itakufuata wewe mwenyewe.

“Haukuwa yule unayelia kwenye mitandao kuwa Lulu amekuibia bwana Majizo lakini ukageuka na kufanya kilekile na unajua jinsi mtu anavyojisikia, Mungu hawezi kubariki furaha yako kwa maumivu ya mwanamke mwingine.”

MOBETTO AKUBALI MATOKEO

Kupitia wimbo wa Barnaba unaoitwa Mapenzi Jeneza, Hamisa alikubali matokeo kwa kunukuu baadhi ya mistari na kuitupia kwenye ukurasa wake wa Snapchat.

Hamisa alisema: “Yatapitaa, vile ulivyonibidua naye unambidua, sa nawaza vile ulivyonihemea naye unamhemea, ni mawazo tu sina plan za kurudi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles