25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Bashiru amtaka Kigwangala kuacha marumbano na Mo

 MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Dk.Bashiru Ally, amemuonya mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega, Dk Hamis Kigwangala, akimtaka kuacha kubishana mitandaoni , badala yake aitumia kukitafutia chama hicho ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao. 

Hatua hiyo ya Dk. Bashiru, imekuja baada ya juzi kuibuka malumbano makali kati ya Kigwangala na mwekezaji wa klabu ya Simba, mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo). 

Mabishano hayo yaliibuka saa chache baada ya Kigwangala ambaye pia ni mwanachama wa Simba, kuhoji vigezo vilivyotumika kumteua Barbara Fernandez kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo. 

Kigwangala kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika: “Nimesikia kuna CEO mpya wa Simba anaitwa Barbara?Kwamba alikuwa msaidizi(PA) wa Moo Dewji?Na pia Mkuu wa Dewji Foundation?Ni kweli?Kama ndivyo, kama mshabiki ningependa kujua elimu yake, uzoefu wake, alivyopatikana!Je hakuna mgongano wa kimaslahi?. 

Baada ya dakika kadhaa, Kigwangala aliandika tena: “Simba siyo NGO,Aidha ipo kwenye transition(kipindi cha mpito) kutoka Club(klabu)kwenda kuwa a ‘corporate entiny’ ya kibiashara. 

Kuna suala la bilioni 20 ya mauzo ya hisa ambazo hazijalipiwa. Je akiwa anatokea kwa msaidizi wa mnunuzi, atatenda haki?Je, ana uwezo wa kuhandle such a complex transction?. “Bodi ya Simba inapaswa kutusaidia kujua ni lini hisa za Simba 50% zililipwa? Na kama hazijalipwa, zitalipwa lini?, na nini kinampa mamlaka MO (ambaye hajalipia 50%) kuwa Mwenyekiti wa Bodi?, kama bodi haina majibu haya wajiuzulu tu. 

 “Kuna ujanja na kuna ujanja ujanja ujanja. Ujanja ni pale Simba tulipokubalian kuhama kutoka kuwa klabu ya wanachama na kuwa na kampuni. Ujanja ujanja ni hiki kinachoendelea sasa , hivi hisa hisa hazijalipiwa PA(Personal assistant) wa mwekezaji ambaye hajalipa hisa anateuliwa kuwa CEO!. 

 “Acha ninyamaze sasa kuna siku ukweli utadhihiri kwa mashabiki na watampiga mawe… mashabiki siyo wa kuchezea chezea,”alisema Kigwangala.

Maandiko hayo yalimwibua Mo ambaye naye kupitia akaunti yake ya Twitter alimjibu Kigwangala kwa kuandika: “Mhe.Kigwangala sio utu kumuombe mtu yeyote apigwe mawe. Suala la uwekezaji Simba nililielezea kwenye mahojiano na Wasafi FM wengi wameelewa, kama bado hutaelewa, namba yangu unayo nipigie nitakufafanulia. Pia nisamehe kwa mkopo wa pikipiki ulioniomba haukuwezekana,” aliandika MO.

Lakini Kigwangala hakuishia hapo, badala yake aliendelea kuandika kwa nyakati tofauti kuhusiana na namna asivyoridhishwa na uwekezaji wa klabu hiyo.

 Marumbano kati ya Kigwangala na Mo yaliwaingiza pia mashabiki wa klabu hiyo, ambao waligawanyika kwenye makundi mawili, wapo waliomuunga mkono Kigwangala kutokana na haua yake ya kuhoji na wapo walionpinga na kumuunga mkono Mo. 

Lakini alimuonya Kigwangala, ambapo kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika hivi: “

“Mheshimiwa Kigwangala naona anazunguka kwenye mitandao kujibizana na, Mohamed Dewji (Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Klabu ya Simba) mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi, mimi nataka nione ana Tweet na wafuasi wake namna mwenyekiti na Rais wetu atakavyoshinda, mwingine anaweza kuona naingilia maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM, hilo muelezeni kabisa,” alisema Dk Bashiru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles