29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

RIHANNA BADO AMUWAZA CHRIS BROWN

 NEW YORK, MAREKANI 

NYOTA wa muziki wa pop nchini Marekani, Rihanna Fenty, amevujisha video ya mwaka 2012 ambayo alihojiwa na Oprah Winfrey na kuweka wazi kuwa bado ana hisia na aliyekuwa mpenzi wake Chris Brown. Video hiyo haikurushwa tangu hapo, lakini wiki hii mrembo huyo aliamua kutumia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuianika kwa mashabiki zake. 

“Mbali ya kuachana, lakini bado tupo kwenye mazungumzo mazuri kama marafiki wa karibu sana, kila mmoja anamuamini mwenzake, kila mmoja anampenda mwenzake na itaendelea kuwa hivyo na haitoweza kubadilika. 

“Najua kwa sasa yeye yupo kwenye uhusiano na mimi sipo kwenye uhusiano, lakini kila mmoja anajua nini analifanya tangu hapo,” alisema Rihanna. 

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi kirefu kabla ya kuachana 2009 kutokana na Chris Brown kumpiga mrembo huyo na kisha kuachana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles