30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA YAIPIGA IHEFU, DODOMA JIJI SAFI

 WAANDISHI WETU 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamezindua vema kampeni zao za kutetea tajila ligi hiyo,baada ya janakuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. 

Mabao yaliyoipa Simba pointi tatu katika mchezo huo, yalipachikwa na John Bocco dakika ya 10 na Mzamiru Yassin dakika ya 42, huku bao pekee la Ihefu likifungwa Omary Mponda dakika ya 14. 

Ushindi huo umefanya Simba kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wa kwanza kwa miaka 13 sasa.

Wekundu hao wa Msimbazi,walipoteza kwa mara ya mwisho mchezo wao wa kwanza 

msimu wa 2007/08, ilipochapwa bao 1-0 na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 

Hata hivyo, haikuwa rahisi kwa Simba kuchomoza na ushindi huo kwani wapinzani wao Ihefu licha ya ugeni wao kwenye ligi, waliwapa changamoto ya kutosha mabingwa hao watetezi. 

Upinzani ulionyeshwa na Ihefu katika mchezo huo, umewasuta wapenzi wengi wa soka walioamini kuwa timu ingeonyesha unyonge nap engine ingefungwa lundo la mabao. 

Kilichoikwamisha Ihefu katika mchezo huo, uzoefu mdogo na mikiki mikiki ya ligi hiyo ukilinganisha na Simba. 

Lakini pongezi bila shaka zitakwenda kwa kocha wa kikosi cha Ihefu, Maka Mwalwisi, ambaye aliifanya timu hiyo kwa nidhamu na ufundi kwa muda wote wa mchezo. 

Licha ya mazingira sehemu ya kuchezea ya uwanja kutoridhisha,timu zote zilijitahidi kucheza soka safi lililoburudisha mashabiki waliojitokeza kwenye uwanja huo. 

Mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake, ilianza kwa kasi, Ihefu ikitumia mipira mirefu kufika langoni mwa Simba. 

Simba ilitumia mfumo wa pasi nyingi na wakati mwingine ndefu kujenga mashambulizi. 

Dakika ya 10, Bocco aliindikia Simba bao la kwanza kwa shuti kali akimalizia pasi ya Mzamiru. 

Dakika ya 14, Mponda alisawazishia Ihefu kwa shuti kali la chini chini lililomshinda mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula. 

Dakika ya 16,mlinda malngo wa Ihefu, Andrew Kayuni alifanya kazi ya ziada kupangua mchomo wa beki wa Simba,Mohammed Hussein na kuzaa kona ambayo 

haikuzaa matunda. 

Dakika ya 19, nusura Enock Jiah aindikie Ihefu bao la pili, baada ya kuachia shuti kali lililopanguliwa na Manula. 

 Dakika ya 30, Bocco alipoteza nafasi ya wazi ambayo angeweza kuiandikia Simba bao, baada ya mpira wake wa kichwa kutua mikononi mwa Kayuni. 

Dakika ya 42, Mzamiru alifungia Simba bao la pili kwa kichwa, akiunganisha pasi ya Clatous Chama. 

Dakika ya 44, mlinzi wa kushoto wa Ihefu, Emmauel Kichiba alilimwa kadi ya njano, baada ya kumkwatua Chama. 

Dakika ya 45, kiungo wa Simba, Hassan Dilunga alilimwa kadi ya njano, baada ya kumkwatua Kichiba. 

Kipindi cha kwanza kilimalizika, Simba ikiwa mbele kwa mabao 2-1. 

Kipindi cha pili, timu zote ziliingia nguvu zaidi zikihitaji ushindi. 

Dakika ya 74, Simba ilifanya mabadiliko, walitoka Bernard Morrison na Dilunga na nafasi zao kuchukuliwa na Ibrahim Ajib na Meddie Kagere. 

Dakika 90 za mtanange huo zilikamilikakwa Simba kutakata kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ihefu. 

Katika michezo mingine,Namungo iliichapa Coastal Union bao 1-0 Uwanja wa Majaliwa, Lindi. 

Biashara United iliikaribissha Gwambina kwa kuichapa bao 1-0, Uwanja wa Karume, Mara, Dodoma Jiji ikailaza Mwadui bao 1-0, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, huku Mtibwa Sugar ikilazimishwa suluhu na Ruvu Shooting Uwanja CCM Gairo, Morogoro. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles