Harrieth mandarin, Geita
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema ni lazima chama hicho kikomeshe tabia ya kufadhiliwa na matajiri badala yake kiendeshwe na miradi ya chama na michango ya hiari na nguvu za wanachama.
Dk. Bashiru ambaye amesema hayo leo Jumatatu Desemba 3, wakati akimaliza ziara yake mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza nidhamu ndani ya chama.
“Tukomeseha tabia ya kutegemea wafadhili badala yake vyanzo vya mapato vianzishwe, michango ya hiari ya wananchama pia ukusanyaji ada za wananchama kwa wakati.
Aidha, amewataka wanachama hao kuacha kupoteza muda kwenye mitandao kwa kuchangia hoja zisizo na tija badala yake washiriki katika shughuli za maendeleo.
“Watu wengi wanapoteza muda kwenye mitandao na sana sana wanayovizungumza ni porojo si mambo ya kujenga, tumekubaliana mwananchama yeyote atakayetumia vibaya mitandao kumhujumu mwenzake, kufitini na kuzua mambo ambayo yanaleta mtafarufu ndani ya chama, vikao vya chama vichukue hatua haraka inavyowezekana,” amesema.
Njia ni moja tu. Turejeshe miko ya uongozi