30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe atatua mgogoro wa ardhi Mvomero

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wananchi wa vijiji vya Kigugu na mbogo Komtonga Wilayani Mvomero Mkoani Morogororo Wanaojishughulisha na kilimo cha Mpunga katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kigugu wameshindwa kuendelea na shughuli za uzalisha wa zao hilo mara baada ya kuelezwa kuwa eneo hilo lipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kitengo Ustawi wa Jamii.

Wakulima hao wametoa kilio chao hicho mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Uvuvi na maji wakati ilipotembelea katika miradi hiyo ili kukagua shughuli zinazoendelea ambapo wamekuta wakulima hao wamesimamisha shughuli za kilimo kutokana na mgogoro huo. 

Akijibu hoja hizo Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe, amewaagiza wakulima kuendelea na shughuli zao za uzalisha wa zao la Mpunga katika Skimu  hiyo ya Uwagiliaji ya Kigugu kwa kuwa wizara haina taarifa juu ya suala hilo .

“Hao waliokuja walikuta hapa kuna mradi wa wizara ya kilimo hivyo kungekuwa na inshu wangekuja kutuona sisi watu wa wizara ya Kilimo,” amesema Bashe.

Hata hivyo ameitaka serikali ya halmashuari ya wilaya ya Mvomero kupima eneo hilo lenye hakari mia nane ili liweze kupewa kwa wananchi wa vijiji hivyo ili kuendelea na uzalishaji wa zao la Mpunga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk. Catherine Ishengoma ameitaka wizara kilimo kuhakikisha inashirikiana haraka na wizara ya afya ili kumaliza sitofahamu hiyo ili wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalisha wa mpunga kwa ufanisi Zaidi.

Kamati hiyo imetembelea miradi ya Skimu ya umwagiliaji pamoja na maghala la kuhifadhia mazao ya Mpunga  katika Wilaya Mvomero na Kilosa,huku ikionyesha kulidhika na ujenzi wa miundombino ya maghala pamoja na Skimu za umwagiliaji zilizojengwa kwa ufadhili wa Bank ya dunia chini ya mradi wa kuongeza uwezo zao la mpunga nchini na kusimamiwa na wizara ya Kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles