24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe ataka wafanyabiashara binafsi wasizuiwe kununua kahawa

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema wafanyabiashara binafsi wakitaka kununua Kahawa wasizuiliwe ambapo amedai Serikali itaendelea kuilinda sekta binafsi na ushirika ili kuwe na usawa katika kilimo.

Pia amesema kama katika sekta binafsi kuna ya shida ya mikopo wanatakiwa kwenda Wizarani ili jambo hilo liweze kutatuliwa.

Akizungumza leo Ijumaa Juni 18,2021 katika mkutano mkuu wa wadau wa zao la kahawa, Bashe amesema wafanyabiashara binafsi wakitaka kununua kahawa wasizuiliwe kwani serikali inataka kuweka uhuru mkulima amuuzie nani zao lake ili aweze kupata faida.

“Wafanyabiashara binafsi wakitaka kununua wasizuiliwe. Niwaombeni viongozi wa vyama vya ushirika msiingie kwenye siasa za majimbo,achaneni na ligi kule Karagwe na jezi mmeandika majina usiruhusu taasisi yako…unaweza ukajikuta unatuhumiwa.

“Ni lazima mkulima anufaike na tunapojadili kilimo ni lazima mkulima anufaike kilimo chetu ni biashara lazima mkulima alime kwa faida,”amesema Bashe.

Aidha,Bashe amesema serikali itaendelea kuilinda sekta binafsi na  ushirika ili kuwe na usawa katika kilimo.

Pia amezitaka bodi ya zao la kahawa kutoa miche yanye ubora kwa wakulima huku akiwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuisimamia miche hiyo 

Hata hivyo, Bashe amewataka Wajumbe wa mkutano huo kutoka na azimio la ni marufuku kwa mkulima kupanda miche chini ya 540 ili mkulima afanye kilimo chenye tija

Vilevile, amewaomba wakurugenzi wa halmashauri asilimia 10 ya mapato yao katika halmashauri kuzipeleka kwenye kilimo kwani huko kumeajiri na kunatoa ajira kwa watu wengi.

Pia, amemwagiza mkuu wa mkoa wa Songwe, Omary Mgumba kuanza kuvishughulikia vyama nane vya ushirika ambavyo vimekula fedha za wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles