28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mashauri 1,208 yatatuliwa na mahakama inayotembea

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mratibu wa Mahakama inayotembea nchini, Hakimu Moses Ndelwa amesema kuwa tangu Julai mwaka 2019 hadi mwezi mei 2021 mahakama hiyo imefanikiwa kutatua mashauri 1208 yaliofunguliwa tokea kuanzishwa kwake.

Alisema huduma hii ilipoanza kutolewa mpaka Mei 2021 jumla ya mashauri hayo 1,208  yalifunguliwa, yakasikilizwa na kumalizika nchi nzima huku kwa upande wa Mwanza pekee wamefanikiwa kusikiliza mashauri 520 na Mashauri yote yalifunguliwa na kumalizika.

Alisema kwa mkoa wa Mwanza asilimia 38% ni  kesi za mashauri ya madai na wafanyabiashara  wadogo ambapo pia mahakama hiyo imefanikiwa kutoa elimu ya ufunguaji mashauri na mpaka mwezi mei mwaka huu walifanikiwa kutoa huduma ya kisheria kwa watu 13,668.

Hakimu Ndelwa alisema mahakama hiyo imejipanga kuhakikisha inasikiliza mashauri ndani ya siku 30 na kutokana na mwitikio  mzuri wa wananchi, Mahakama yao inaangalia uwezekano wa kutanua wigo wa kutoa huduma ya Mahakama inayotembea hususani maeneo ya vijijini.

Aidha alisema kuwa mahakama hiyo imejipanga kuzifikia wilaya zote  ambazo hazina majengo ya mahakama ya wilaya ikiwemo wilaya za Shirati, Butiama, Gairo, Chamwino na Chemba.

Alieleza, tathimini ndogo inaonyesha kwa huduma ya mahakama inayotembea imesaidia mwananchi kuokoa hadi Sh 300,000 ambazo ni pesa za usafiri kwa shauri moja.

Kwa upande wake Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Monica Onesmo alisema Mahakama hiyo imesaidia sana kupunguza msongamano wa mashauri.

Mkazi wa kata ya Mkolani Cloud Seseja alisema mahakama hiyo inasaidia kukomboa wakati na huduma zao ni nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles