Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii ili kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa ukililenga Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Soma zaidi… http://mtanzania.co.tz/serikali-yawatikisa-maaskofu-wa-kkkt/
Waziri Nchemba amesema hayo leo Ijumaa Juni 8, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Huo waraka una maudhui kama matatu, ni waraka batili na tunaendelea kuchunguza kama umeyengenezwa basi umetengenezwaje, kwani haujapita kwetu.
“Hivyo basi, namsimamisha Msajili wa hizo taasisi kupisha uchunguzi na ikithibitika ni za Wizara tuweze kujua maana jambo hilo halijapita kwa Waziri, Katibu Mkuu na wala si maelekezo ya serikali,” amesema.
Hata hivyo, Waziri Mwigulu aliuita waraka huo ni batili kwa kuwa haukukidhi viwango vya uandishi wa nyaraka za serikali.