26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Barnaba: Tusiwatenge watoto wenye ulemavu

BARNABANA RUTH MNKENI
WIMBO wa ‘Tuwapende’ wa msanii wa Bongo Fleva, Barnaba umetumika katika kampeni ya kuhamasisha jamii isiwatenge watoto wenye ulemavu wa akili.
Barnaba alionyesha kwa vitendo kuhamasisha jamii hiyo kupitia wimbo wake huo huku akicheza na baadhi ya watoto hao waliokuwa wamekusanyika katika matembezi hayo mwishoni mwa wiki.
“Mimi kwa kweli niliguswa ndiyo maana nikatoka na wimbo huo kwa kuwa naamini hakuna mtu anayependa kupata mtoto mwenye ulemavu wowote na ikitokea hivyo huwa ni mapenzi ya Mungu,” alieleza Barnabas.
Barnabas alikuwa balozi katika matembezi hayo yaliyoandaliwa na Balozi wa kujitegemea wa kuhamasisha jamii kutowatenga watoto wenye matatizo ya akili, Emanueli Likuda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles